Home Sports KUMBE MAYAY ALISHTUKIZWA UBOSI

KUMBE MAYAY ALISHTUKIZWA UBOSI

LEGEND wa soka Bongo, Ally Maya Tembele amebainisha kuwa taarifa za kuteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Tanzania zilimfikia kwa kustukizwa na hakuwa na tetesi za kuwa atapewa nafasi hiyo.

Septemba 20 Mayay aliteuliwa kuchukua nafasi ya Yusuph Singo aliyepangiwa majukumu mengine.

Mayay alibainisha hayo alipokuwa mubashara kwenye kipindi cha Krosi Dongo kinachorushwa kila siku kupitia +255 Global Radio na Global TV.

Mayay amesema:”Kiukweli sina taarifa, wewe ndiye unanipa ‘breaking news’ hii sina taarifa kabisa na ninakosa hata jambo la kuongea na kuzipokea pongezi hizo ambazo unanipa, Imenishtua sana habari hii unayonipa.

“Sikuwa na tetesi na sikuwahi kugusiwa kuwa nafikiriwa kupewa nafasi hiyo kubwa ya uongozi ya masuala ya uongozi wa masuala ya michezo nchini. Lakini naweza kusema asante kwa nafasi hiyo kama kweli kwa sababu ni jambo kubwa kwangu hata kama nimeteuliwa kwa kushtukiza,” alisema Mayay.

Previous articleMBINU 4, AL HILAL WANAKUFA, KOCHA MSAUZ AOMBA KAZI SIMBA
Next articleWAZAWA SIMBA WANSTAHILI PONGEZI KWA WALICHOKIFANYA