SIMBA YAANZA KWA USHINDI KIMATAIFA

JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba ameanza kazi yake kwa mara ya kwanza kwenye mashindano a kimataifa katika Ligi ya Mabingwa Afrika na timu hiyo imeshinda mabao 2-0 dhidi ya ig Bullets.

Mchezo huo wakiwa ugenini Uwanja wa Bingu, kipindi cha kwanza Simba walianza kupata bao la kuongoza kupitia kwa Moses Phiri dakika ya 28.

Bao hilo lilidumu mpaka muda wa mapumziko na kipindi cha pili walipata bao la pili kupitia kwa nahodha John Bocco.

Mgunda amesema kuwa wachezaji wake wamepambana na kupata ushindi kwenye mchezo huo uliokuwa ni mgumu kwa timu zote mbili.

“Ninafurahi kuona vijana wamepata matokeo na haukuwa mchezo rahisi ila wachezaji wamepambana na kupata ushindi bado kuna kazi kwenye mechi zijazo kimataifa tutafanyia kazi makosa yetu,” amesema Mgunda