SIMBA YAPOTEZA MCHEZO WA KIMATAIFA

KIKOSI cha Simba leo kimepoteza mchezo wa kirafiki kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Arta Solar uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Bao pekee la ushindi kwa Arta Solar lilipachikwa dakika ya 89 kupitia kwa nyota wao Manunchu Athuman ambaye aliweza kupachika bao hilo lililomshinda kipa Ally Salim.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza Simba walifanikiwa kutawala kwenye mchezo huo kwa kutengeneza nafasi walizokwama kuzitumia.

Mzawa Moses Kitandu ni miongoni mwa wachezaji wa Arta Solar ambaye alipata nafasi ya kucheza leo akitokea benchi.

Kabla ya mchezo huo wachezaji na mashabiki waliweza kusimama kimya kumuombea Dkt.Yassin Gembe ambaye ametangulia mbele za haki alikuwa akifanya kazi Simba.

Kocha Mkuu wa Simba, Zoran Maki amesema kuwa walishindwa kutumia nafasi ambazo walizipata kwenye mchezo huo na waliwakosa baadhi ya wachezaji waliokuwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania.