KOCHA Mkuu wa Newcastle United, Eddie Howe amesema kuwa hajaelewa mpaka sasa kwa nini ziliongezwa dakika nyingi kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu England dhidi ya Liverpool.
Ni mabao 2-1 walifungwa kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Anfield na bao la ushindi lilifungwa dakika za lala salama.
Ni Fabio Carvalho alifunga bao la ushindi dakika ya 90+8 kwenye mchezo huo ambao Newcastel United walikuwa wanaamini kwamba wangepata pointi moja ugenini.
Alipachika bao hilo zikiwa zimepita dakika tatu kutoka dakika tano ambazo ziliongezwa kwenye mchezo huo jambo lililoleta malalamiko.
“Mpaka sasa ningehitaji mtu anifafanulie kwa kuwa mimi niliyekuwa nimekaa,(kwenye benchi) sielewi.
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema wachezaji wa timu pinzani walicheza kwa mbinu ya kupoteza muda