BAO la ushindi ambalo alifunga Jadon Sancho kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Leicester City wakiwa ugenini limemfanya achaguliwe kuwa mchezaji bora wa mchezo huo.
Ilikuwa ni Uwanja wa King Power Manchester United walifanikiwa kukusanya pointi tatu wakiwa ugenini.
Ushindi huo unaifanya timu hiyo kufikisha jumla ya pointi 9 ikiwa nafasi ya tano kwenye msimamo na Leicester City wao wapo nafasi ya mwisho kwenye msimamo wakiwa wamekusanya pointi moja baada ya kucheza mechi 5.
Ni mashuti 10 walipiga kuelekea kwenye lango la Manchester United Leicester City na ni mawili yalilenga lango na kwa upande wa United wao walipiga mashuti 9 na mawaili yalilenga lango.