KIKOSI cha Simba leo kitakuwa na kazi ya kusaka ushindi dhidi ya Al Hilal ukiwa ni mchezo wa kimataifa wa kirafiki wakiwa nchini Sudan.
Utakuwa ni mchezo wa pili leo baada ya ule wa awali kuweza kushinda mabao 4-2 Asante Kotoko.
Seleman Matola, Kocha Msaidizi wa Simba ameweka wazi kuwa mchezo wa leo ni muhimu kwao kuendelea kukitazama kikosi hicho ambacho kinafanya maandalizi kwa ajili ya msimu mpya wa 2022/23.
“Haya ni mashindano muhimu kwetu na tunayachukulia kwa umuhimu mkubwa, kila mmoja anatambua kuwa kwa sasa mwalimu anaunda kikosi cha ushindani.
“Mchezo uliopita wachezaji wengi walipata nafasi ya kuonyesha uwezo wake hasa wale ambao walikuwa hawapati nafasi kwenye mechi zilizopita hivyo bado tuna kazi yakufanya kuwa na kikosi kizuri,” amesema.