SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema mchezo wa leo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Al Hilal ya Sudan ni muhimu kwao kuzidi kupata ushindi.
Mchezo wa leo unakuwa ni wapili baada ya ule wa awali kushinda mabao 4-2 dhidi ya Asante Kotoko na nyota wa mchezo akiwa ni Clatous Chama aliyefunga mabao mawili.
Pia kuna nyota wawili ambao wamengezeka kwenye kikosi hicho awali hawakuwa kwenye kikosi nchini Sudan.
“Imekuwa vizuri kwetu kupata ushindi kwenye mchezo ule wa kwanza na sasa tunakwenda kucheza mchezo wa pili ambao ni muhimu kwetu kushinda.
“Wachezaji wengine wameongezeka ikiwa ni Sadio Kanoute ambaye alikosekana kwenye mchezo wa kwanza pamoja na John Bocco ambaye hakuwa pia kwenye kikosi mchezo uliopita.
“Tunahitaji ushindi na tunawaheshimu wapinzani wetu kwenye mchezo wetu tutapambana kushinda,” amesema.