KOCHA WA MABINGWA WA LIGI YA MABINGWA ULAYA AONYA

 BOSI wa mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya amewaonya mastaa wake kwa kuwaambia kwamba wanapaswa kuongeza umakini.

Carlo Ancelotti amewaambia wachezaji wake kwamba wanapaswa kuongeza umakini kutokana na mazingira ambayo wapo kiushindani.

Timu hiyo imepangwa Kunid F na timu za RB Leipzig, Shakhar Donetsk na Celtic.

Kocha huyo anakumbuka kwamba msimu uliopita timu hiyo ilinyooshwa mabao 2-1 dhidi ya FC Sheriff wakiwa nyumbani, Uwanja wa Santiago Bernabeu.

Kocha huyo amesema:”Tumepangwa katika kundi tofauti kabisa kumbuka miezi miwili iliyopita tumecheza karibu kila kwenye mchezo kwenye michuano hii tulipoteza Bernabeu dhidi ya Sheriff.

“Ndiyo maana tunahitaji kuwa makini, kwani yatakuwa mazingira magumu kabisa na haitakuwa rahisi kucheza Glasgow na pale Leipzig, kwa maana hiyo tunatakiwa kuwaheshimu wapinzani wetu,” amesema.