GWIJI wa Liverpool, Luis Suarez, amemuonya Mruguay mwenzake, Darwin Nunez kujifunza kutoka kwenye makosa yake baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumpiga kichwa Joachim Anderson kwenye sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Crystal Palace.
Mshambuliaji huyo anayeichezea Nacional kwa sasa anakumbukwa kwamba alikuwa ni mbabe na mtukutu katika miaka mitatu ambayo alitumika ndani ya Liverpool.
Nyota huyo amefichua kwamba amezungumza na Nunez na kumpa ushauri kufuatiwa kutolewa nje kwa kadi kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.
“Nimezungumza naye kwa sababu ndiyo kwanza anaanza na nilitaka kumfanya ajue kwamba kwa sasa, (wapinzani) watakuwa wanamfuata mara mbili au tatu hata zaidi,” amesema.