CASEMIRO HUYO MAN UNITED

MANCHESTER United imekubaliana na Real Madrid dili la kumsajili kiungo Casemiro kwa pauni milioni 60.

Tayari pande zote zimeshakubaliana huku United pia ikiwa imeshakubaliana na Mbrazil huyo ambaye anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya wikiendi hii kabla ya kusaini mkataba wa miaka minne, Old Trafford.

Mkataba huo unakipengele cha kuongeza mwaka mwingine zaidi ikiwa atafanya kazi nzuri na kubwa.

Casemiro alimueleza kocha Carlo Ancelotti kuhusu uamuzi wake wa kutaka kujiunga na United baada ya kukutana kwa mazungumzo na kuzungumza kuhusu masuala yake ya kubaki ama kuondoka ndani ya kikosi hicho.