Home Sports YANGA YAINGIA MKATABA WA MIAKA MIWILI NA JACKSON GROUP

YANGA YAINGIA MKATABA WA MIAKA MIWILI NA JACKSON GROUP

KLABU ya Yanga leo Agosti 19,2022 imeingia makualiano na Kampuni ya Masoko iitwayo Jackson Group.

Kwa mujibu wa rais wa Yanga,  Hersi Ally Said amesema kuwa  wameingia mkataba wa miaka miwili na Kampuni ya masoko ya Jackson Group ambayo itakuwa na jukumu la kuleta mahusiano ya kibiashara kati ya Yanga na washirika wengine.

“Kampuni ya Jackson Group ni kampuni ya Watanzania wenzetu ikiendeshwa na CEO na Kelvin Twissa historia yake inajieleza ni mtu wa namna gani katika uwanja huu wa masoko.

“Ajenda moja wapo wakati nilivyoingia madarakani ilikuwa ni kutengeneza mfumo ambao utakwenda kuifanya klabu hii kuwa moja ya vilabu vikubwa Barani Afrika, tukio la kusaini Mkataba na Jackson Group unaakisi uelekeo wa imara wa kifedha wa Klabu kwa kuleta wadhamini zaidi kwenye klabu yetu kupitia kampuni hii ambayo ina uzoefu mkubwa katika sekta hiyo.

Twisa amesema kuwa mkataba huo ni wa manufaa kwa pande zote mbili na wanaamini kila mmoja atapata faida kwenye  biashara.

“Mpira ni biashara na kupitia makubaliano haya nina amini kwamba kila mmoja atapata faida na tumeweza kukubali kufanya kazi na Yanga kwa kuwa ina viongozi bora na tuna imani ya kufanya nao kazi,” amesema.

 

Previous articleKILA MTU ANA NAFASI YA KUSHINDA JACKPOT MERIDIANBET, UNAFAHAMU JACKPOT NI NINI NA NAMNA YA KUSHINDA?
Next articleSAUTI:ISHU YA MANZOKI KUIBUKA SIMBA MAPYA YAIBUKA