NUNEZ AOMBA RADHI

DARWIN Nunez, mshambuliaji wa Liverpool ameomba radhi kwa kitendo chake cha kumpiga kichwa beki wa Crytal Palace, Joachim Andersea akisisitiza kuwa amejifunza kutokana na makosa.

Tukio hilo lilitokea kwenye mchezo wa Liverpool dhidi ya Crystal Palace uliochezwa Uwanja wa Anfield, juzi Jumatano na kwa tukio hilo nyota huyo alitolewa kwa kadi nyekundu.

Ni mchezo wa kwanza kwa Nunez akiwa nyumbani mbele ya mashabiki wa Liverpool ikiwa ni ingizo jipya kutoka Benfica.

“Naomba radhi nimejifunza kutokana na makosa haitajirudia tena, nimejifunza kwa sasa nilichokifanya sio sahihi najua,” .

Mchezo huo ulikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1 ambapo bao la Liverpool lilifungwa na Luis Diaz dk ya 61 na lile la Crystal Palace lilifungwa na Wilfried Zaha dk ya 32.