Home Sports MANULA KUIKOSA YANGA KESHO KWA MKAPA

MANULA KUIKOSA YANGA KESHO KWA MKAPA

KIPA namba moja wa Simba, Aishi Manula kesho anatarajiwa kuukosa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga kutokana na kuwa bado hajawa fiti.

Manula alipata maumivu kwenye mchezo wa kimataifa wa timu ya Taifa ya Tanzania dhidi ya Somalia uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa Simba, Zoran Maki amesema kuwa bado Manula hajapona.

“Aishi Manula bado hajapona hivyo kuhusu kuanza kwake bado hataweza kuanza mchezo wa kesho labda ikitokea jambo lingine.

“Lakini ambacho tunakifanya kwa sasa ni kuweza kujiandaa vizuri ili kuweza kupata ushindi kwani tunatambua kwamba mchezo utakuwa mgumu na ushindani mkubwa,” amesema.

Kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya St George,Manula hakuweza kuanza kikosi cha kwanza kwenye mchezo huo na badala yake alianza Beno Kakolanya.

Previous articleMAPILATO YANGA V SIMBA HAWA HAPA
Next articleJESUS MOLOKO KAMILI KUIVAA SIMBA,KAMBOLE BADO