Home Sports JESUS MOLOKO KAMILI KUIVAA SIMBA,KAMBOLE BADO

JESUS MOLOKO KAMILI KUIVAA SIMBA,KAMBOLE BADO

JESUS Moloko kiungo wa Yanga kesho anatarajiwa kuweza kucheza kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Kiungo huyo alikwama kuanza kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Vipers SC ya Uganda wakati Yanga ilipopoteza kwa kufungwa mabao 2-0 Uwanja wa Mkapa.

Nasreddine Nabi,Kocha Mkuu wa Yanga amebainisha kwamba watacheza kwa umakini mchezo wa kesho na jukumu la benchi la ufundi ni kuangalia nani ataweza kuanza.

“Jesus Moloko alikosekana kwenye mchezo dhidi ya Vipers kwa kuwa alipata maumivu kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo FC uliochezwa Kigamboni.

“Hata Lazalous Kambole naye alipata maumivu lakini huyu bado hajawa fiti zaidi isipokuwa Moloko yeye anaweza kuanza kwenye mchezo wa kesho kwa kuwa yupo vizuri.

“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho ili kuweza kupata matokeo tumepata muda wa kufanya maandalizi kwa ajili ya mchezo wetu wa Ngao ya Jamii na tunatambua kwamba utakuwa na ushindani mkubwa,” amesema.

Previous articleMANULA KUIKOSA YANGA KESHO KWA MKAPA
Next articleVIDEO:MAKI AZUNGUMZIA KUHUSU AISHI MANULA,BOCCO ATOA NENO