Home Sports HIKI HAPA KIKOSI KIPYA CHA KMC,MASTAA WAPYA 14

HIKI HAPA KIKOSI KIPYA CHA KMC,MASTAA WAPYA 14

KIKOSI cha KMC FC kinachoshiriki Ligi Kuu Bara, msimu ujao kitakuwa na jeshi la wachezaji 27 kati yao nyota 14 ni wapya.

KMC msimu uliopita ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya 10 na pointi 35 baada ya kucheza mechi 30 huku Kocha Mkuu, Hitimana Thiery akibaki na nyota 13 aliokuwa nao msimu uliopita wa 2021/22.

Ofisa Habari na Mawasiliano wa KMC, Christina Mwagala amewataja nyota wapya kuwa ni;”George Makang’a, Ibrahim Ame, Baraka Majogoro, Isaac Kachwele, Steve Nzigamasabo, Bigirimana Blaise,Boniphace Maganga.

 “Daruweshi Saliboko, Waziri Junior, David Kisu, Nourdine Balora, Erick Costantine, Farshad Mogela pamoja na Balisi Maliki.

“Kuhusu Juma Kaseja ambaye ni kipa wetu wa muda mrefu na mwenye uzoefu mkataba wake umefika ukingoni tunazungumza naye tutatoa taarifa,” amesema Mwagala.

Kikosi hicho kinaendelea na maandalizi ya msimu mpya ambapo Agosti 17 kitashuka Uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga kuwakabili wenyeji wao Coastal Union.

Previous articleKUMUONA AZIZ KI,MORRISON,OKWA BUKU TANO
Next articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI