Home Sports SIMBA KUMENYANA NA BIG BULLETS

SIMBA KUMENYANA NA BIG BULLETS

WASHINDI namba mbili wa Tanzania kwenye Ligi Kuu Bara, Simba wataanza ugenini kumenyana na Big Bullets ya Malawi.

Hiyo itakuwa ni kwenye hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika inayotarajiwa kuchezwa kati ya Septemba 9-11.

Mshindi wa mchezo huo anaweza kukutana na mshindi wa mchezo kati ya Red Arrows ama De Agosto ya Angola.

Droo hiyo imepangwa leo Agosti 9,2022 nchini Misri yalipo makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika,(CAF).

Previous articleYANGA KIMATAIFA KUANZA NA ZALAN FC
Next articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO