Home Sports M BET TANZANIA YAFURAHISHWA NA TAMASHA LA SIMBA DAY

M BET TANZANIA YAFURAHISHWA NA TAMASHA LA SIMBA DAY

KAMPUNI ya michezo ya kubahatisha ya M-BET Tanzania imevutiwa na kufana kwa tamasha la Klabu ya Simba (Simba Day) ambalo  lilifanyika Jumatatu (Agosti 8, 2022) kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mbali ya utambulisho wa wachezaji kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Kombe la Azam Federation na Ligi ya Mabingwa Afrika, tamasha hilo pia ni sehemu ya kusheherekea siku ya kuanzishwa kwa klabu hiyo.

Mkurugenzi wa Masoko wa M-BET, Allen Mushi amesema kuwa wamefarijika jinsi tamasha hilo lilivyoandaliwa na kufanyika kwake kiasi cha mashabiki kuujaza Uwanja wa Benjamin Mkapa ambao unaingiza jumla ya watu 60,000.

Mushi amesema kuwa M-BET ilikuwa inajumuika kwa mara ya kwanza tangu kuwa mdhamini mkuu wa klabu hiyo na jinsi mambo yalivyoendeshwa yalikuwa yenye weledi wa hali ya juu, japo katika kila jambo lazima kutakuwa na mapungufu.

“Ukiachana na changamoto mbalimbali, tamasha lilikuwa la kufana sana, mashabiki wengi walifika na mbali ya kushuhudia timu hiyo ilishinda mabao 2-0, burudani za wasanii mbalimbali ziliwaburudisha mashabiki hao ambao walianza kuingia uwanjani kuanzia saa 2.00 asubuhi,” amesema Mushi.

M-BET Tanzania imesaini mkataba wa miaka mitano na  Klabu ya Simba wenye thamani ya Sh bilioni 26.1 na kuwa wadhamini wakuu wa klabu hiyo.

Udhamini huo unaiifanya Klabu ya Simba kuwa na thamani kubwa kuliko zote nchini kutokana na kiasi kikubwa cha fedha.

Mwaka wa kwanza wa mkataba wao, M-BET wataipa Simba sh 4,670,000,000 ambapo kiasi hicho kitaongezeka msimu wa pili ambapo Simba itapata sh 4.9 bilioni na mwaka wa tatu wataipa Simba Sh bilioni 5.2.

M-BET itazidi kuiongezea Simba fedha kwani mwaka wanne wataipa Sh5.5 billioni na mwaka wa tano kiasi cha sh 5.8 bilioni itapewa Simba.

Previous articleHIKI HAPA KIKOSI CHA YANGA MSIMU WA 2022/23
Next articleCAF KUFANYA MKUTANO WAKE ARUSHA