ZIKIWA zimebaki siku 6 kabla ya watani wa jadi kukutana kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii,Agosti 13 ipo wazi kuwa makocha wote wawili wataibiana mbinu.
Ni mchezo wa Yanga v Simba ambao unasubiriwa kwa shauku kubwa na timu zote zinahitaji ushindi kwa kuwa hakuna sare katika mchezo huo.
Nasreddine Nabi,Kocha Mkuu wa Yanga atakuwa wa kwanza kuuza mbinu zake mbele ya Zoran Maki wa Simba itakuwa ni Agosti 6 kwenye mchezo wa Wiki ya Mwananchi ambapo Yanga itacheza na Vipers FC.
Vipers FC ya Uganda inatarajiwa kuwasili nchini leo ili waweze kufanya maandalizi ya mwisho kabla ya kumenyana na Yanga katika Wiki ya Mwananchi iliyopewa slogan ya Yanga ByutiByuti.
Nabi akishamaliza kuuza mbinu kwa Maki yeye atakuwa na kazi ya kuweza kuzisoma mbinu za kocha mpya wa Simba kwenye mchezo wao wa Simba Day,Agosti 8 ambapo wanatarajiwa kucheza na St George.
Nabi amesema kuwa kabla ya mchezo unaoihusu timu yake ni lazima aweze kuangalia namna wapinzani wake wanavyocheza.
Maki amesema kuwa ni muhimu kuwatambua wapinzani kabla ya mchezo ili kuweza kupanga kikosi cha ushindi.