SELEMAN Matola,Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa usajili ambao umefanywa kwa ajili ya maboresho ya kikosi hicho kunawafanya warudi msimu ujao wakiwa na kasi nyingine.
Nyota sita wametambulishwa Simba ikiwa ni wazawa wawili ambao ni Habib Kyombo na Nassoro Kapama huku wageni ikiwa ni Moses Phiri, Mohamed Outtara,Victor Ackpan,Auhgustine Okra.
Matola amesema kuwa kwa namna ambavyo usjili umefanyika na kiu ya wachezaji kufanya vizuri inawapa nguvu ya kuweza kurejea kwenye ubora wao.
“Usajili ambao umefanyika ni maalumu kwa ajili ya zile nafasi ambazo zilikuwa zina mapungufu hivyo kwa sasa unaona kwamba kila nafasi imeweze kufanyiwa kazi na hilo linatufanya tuweze kuwa kwenye ubora wetu msimu ujao.
“Ile Simba ambayo ilikuwa inapendwa na wengi inarejea na hata ujio wa kocha mpya nao unaongeza kitu hasa ukizingatia kwamba mwalimu,(Zoran Maki) naye ni muumini wa mpira ule unaopendwa hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,” amesema Matola.
Simba imeweka kambi Misri kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2022/23 inatarajiwa kurejea Bongo Agosti 3 kwa ajili ya maandalizi ya Simba Day,Agosti 8.