Home Sports MKATABA WA SIMBA NA M-BET BILIONI 26

MKATABA WA SIMBA NA M-BET BILIONI 26

MTEDAJI Mkuu wa Simba,Barbara Gonzale amesema kuwa leo ni kubwa kwa Simba na kampuni ya kubashiri ya M-Bet ambao ni wadhamini wao wakuu walioweka mkwanja mrefu kwa muda wa miaka mitano.

Ni mkataba wenye thamani ya bilioni 26 kwa miaka mitano ikiwa ni mkwanja mrefu watakaopokea Simba kwa mafungumafungu.

Barbara amesema:”Leo ni siku kubwa kwa Simba na M-Bet. Swali kubwa ni kwanini M-Bet. Sababu kubwa ni wameweza kukidhi mahitaji yetu.

“Kwa ukubwa wa Simba ni lazima kujihusisha na kampuni ambayo inaongoza kwenye biashara ambayo wanafanya. Mkiangalia takwimu M-Bet wanaongoza kwa ukubwa Tanzania.

“Washirika wote wa Simba kwa sasa wamejitoa kwa Simba tu.Hii ni mara ya kwanza mdhamini mkubwa anakuwa na senior team pekee, huko nyuma mdhamini mkuu alikuwa kwa timu zote lakini sasa timu zingine tunaweza kuzitafutia mdhamini wake.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Masoko wa M-Bet Allen Mushi amesema:”M-Bet ni kampuni namba moja ya michezo ya kubashiriki sasa tunashirikiana na klabu namba moja Tanzania.Tunaamini kama M-Bet tukishirikiana na Simba tutajitangaza ndani na nje ya Tanzania.”

“Mwaka wa kwanza – Bil 4.670
Mwaka wa pili – Bil 4.925
Mwaka wa tatu – Bil 5.205
Mwaka wa nne – Bil 5.514
Mwaka wa tano – Bil 5.853

Jumla ni Bilioni 26, milioni 168 na Tsh. 5,000.”

Previous articleMENEJA MPYA YANGA ATOA SHUKRANI ZAKE KMC
Next articleSAUTI:AZAM FC KAZI INAENDELEA,WAKAMILISHA ICT