HUSSEIN Massanza,Ofisa Habari wa Singida Big Stars ameweka wazi kuwa maandalizi kwa ajili ya msimu ujao wa 2022/23 yanakwenda vizuri.
Timu hiyo ambayo imepanda Ligi Kuu Bara kutoka Championship kwa sasa imeweka kambi Mjini Arusha kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.
Imebadili jina kutoka DTB mpaka kuwa ni Singida Big Stars kutokana na sababu za kibiashara.
“Maandalizi kwa ajili ya msimu ujao yanakwenda vizuri na kila mchezaji anatimiza majukumu yake na tunatambua kwamba ushindani utakuwa mkubwa tupo tayari,”.
Miongoni mwa wachezaji ambao wamesajiliwa ndani ya Singida ni pamoja na Said Ndemla,Yassin Mustapha,Paul Godfrey wanaungana na mastaa wengine ikiwa ni pamoja na Juma Abdul,James Kotei.