Home Sports TAIFA STARS MNA DENI KWA WATANZANIA,INAWEZEKANA

TAIFA STARS MNA DENI KWA WATANZANIA,INAWEZEKANA

ILIKUWA ngumu kuweza kupata ushindi kwenye mchezo wa kwanza kutokana na mbinu kuonekana kuwa ngumu pia kwa timu zote mbili.

Hakika kwa mwanzo mkiwa nyumbani licha ya kwamba Somalia wao walikuwa wenyeji bado wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars mna deni la kulipa.

Hakika mashabiki wanapeda kushangilia na kuona matokeo yanapatikana kwa mabao mengi zaidi ya mawili na hili lipo kwenye miguu yenu.

Kazi ya kwanza mwendo wake umegota ukingoni bado kazi ya pili ambayo itakuwa ngumu zaidi ya ile ya awali pale Uwanja wa Mkapa.

Ikumbukwa kwamba mchezo wa marudio upo njiani na kila mchezaji anatambua kwamba ushindi kwenye mchezo huo wa kuwania kufuzu CHAN nchini Algeria ni muhimu.

Kwa namna moja ama nyingine tunajua kwamba hakuna ambaye alitarajia kwamba mngekutana na ushindani ule kwa wapinzani hii inatokana na kwamba mlikuwa mpo nyumbani.

Imani yetu ni kwamba kwa namna ambavyo mchezo wa kwanza ulikuwa benchi la ufundi limeona wapi ambapo litakwenda kuboresha kwa ajili ya mechi ijayo ambayo inatarajiwa kuchezwa Julai 30.

Kila kitu kinawezekana kikubwa ni maandalizi na matumizi ya nafasi ambazo zitapatikana kwenye mchezo wenu ujao na hili kwenu wachezaji.

Matumizi ya nafasi ambazo mtazipata ni muhimu kwenu kwa kuwa hakuna nafasi nyingine ambayo mtaipata tena mkipoteza nafasi moja.

Previous articleSINGIDA UNITED CHIMBO LAO ARUSHA
Next articleMANARA:SIHITAJI KUONEWA HURUMA