ABDIHAMID Moallin, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa wanatarajia kucheza mechi nyingi za kirafiki nchini Misri ambapo wataweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2022/23.
Kesho Ijumaa,Julai 22 kikosi cha Azam FC kinatarajia kukwea pipa kuelekea Misri kwa ajili ya kambi ya siku 20.
Kocha huyo ameweka wazi kuwa program ambazo alianza nazo zimewapa mwanga wa kujua nini watafanya kwa msimu ujao huku akiamini kwamba watakuwa kwenye mwendo mzuri.
“Tumeanza na program ya asubuhi kuwa gym na jioni uwanjani ili kuwaweka fiti kwani walikuwa na likizo kidogo pia tunawaandaa kisaikolojia ili kuwa sawa kuelekea msimu ujao,”.
Ikumbukwe kwamba Azam FC ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 30 msimu wa 2021/22.
Ni pointi 49 ilikusanya kibindoni huku vinara wakiwa ni Yanga waliokusanya pointi 74.