UONGOZI wa Azam FC umefunga usajili wao kwa kumtambulisha beki wa kati wa kimataifa raia Senegal, Malickou Ndoye, akitokea Teungueth FC ya huko.
Taarifa iliyotolewa na Azam FC imeeleza kuwa Ndoye mwenye miaka 22, ni mmoja wa mabeki wanaokubalika na Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Senegal, Aliou Cisse ambaye alimjumuisha kwenye kikosi kilichoshiriki COSAFA nchini Afrika Kusini mwaka huu.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC,Zakaria Thabit amesema kuwa usajili huo unahitimisha zoezi la usajili.
Nyota huyo anakuwa ni wa tisa ndani ya Azam FC akiungana na Kipre Junior, Tape Edinho, Isah Ndala, Nathaniel Chilambo, Cleophace Mkandala, Abdul Sopu, James Akaminko na mlinda mlango Ali Ahamada.
Jana,Julai 19 2022 kikosi cha Azam FC kiliweza kuanza kambi ya ndani kabla ya ile ya kuelekea Misri ambapo watakuwa huko kwa muda wa siku 20.