SIMBA DAY NI AGOSTI 8,2022

 AGOSTI 8,2022 inatarajiwa kuwa siku rasmi ya Simba Day ambayo itafanyika Uwanja wa Mkapa.

Siku hiyo ni maalumu kwa ajili ya utambulisho wa wachezaji wa Simba pamoja na benchi la ufundi la timu hiyo ambayo kwa sasa ipo chini ya Kocha Mkuu,Zoran Maki.

Timu hiyo imeweka kambi nchini Misri ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2022/23 ikiwa na mastaa wake wapya iliyowasajili.

Miongoni mwa wachezaji hao ni pamoja na Augustino Okra,Moses Phiri,Victor Ackpan,Nassoro Kapama na Habib Kyombo.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba,Ahmed Ally amesema kuwa watakaporejea kutoka Misri itakuwa ni kufanya maandalizi ya mwisho ya Simba Day kisha kazi ya mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga.