JUVENTUS YAKUBALI KUMUUZA BEKI WAO

KLABU ya Juventus ya Italia imekubali kumuuza beki wake wa kati, Matthijs de Ligt (22) kwenda  kwa mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich kwa ada ya Paundi Milioni 68 (Tsh. 186,320,000,000)

Taarifa kutoka Ujerumani zinaeleza kuwa beki huyo wa kimataifa wa Uholanzi atasaini mkataba wa miaka mitano na Bayern mara baada ya kukamilisha vipimo vya afya anavyotarajia kufanya leo katika jiji la Munich.

De Ligt anaondoka Juventus akiwa amekaa kwa misimu mitatu, akicheza mechi 177 na kufunga magoli nane. pia, alishinda taji la Serie A katika msimu wa 2019/20.