AZAM FC YATAMBIA USAJILI WAO

UONGOZI wa Azam FC, umeweka wazi kuwa usajili ambao wameufanya kwa ajili ya msimu mpya wa 2022/23 umezingatia mapendekezo ya benchi la ufundi kwa asilimia kubwa.

Tayari Azam FC imewatambulisha mastaa 8 ikiwa ni pamoja na Cleophance Mkandala kutoka Dodoma Jiji,Isah Ndala kutoka Plateau United,Tape Edinho kutoka ES Bafing,Kipre Junior kutoka Sol FC.

Pia yupo kiungo Abdul Suleiman,’Sopu’ kutoka Coastal Union,Nathaniel Chilambo kutoka Ruvu Shooting,Ali Ahamada alikuwa mchezaji huru na James Akaminko kutoka Grea Olympic.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa usajili ambayo umefanyika umezingatia mahitaji ya timu pamoja na ripoti ya benchi la ufundi.

“Inapofikia suala la usajili Azam FC huwa tunakuwa tofauti kabisa,tunaangalia ripoti ya benchi la ufundi na mahitaji ya timu kisha tunawafuatilia wachezaji ambao tunawahitaji na sio suala la siku moja.

“Wapo wachezaji ambao huwa inatuchukua zaidi ya misimu miwili kuwafuatilia kutokana na sababu mbalimbali huwa inatufanya tunawakosa lakini haina maana kwamba huwa tunashindwa hapana kwenye jambo letu huwa tunatimiza,” amesema Zakaria.

Kwa sasa Azam FC inasaka beki mmoja wa kazi kwa ajili ya kuwa naye kwenye msimu mpya wa 2022/23 ndani ya Ligi na Kombe la Shirikisho Afrika.