YEYE ni mchezaji bora wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2021/22 ambapo kasepa na tuzo tatu mazima msimu huu.
Ni tuzo ya kiungo bora baada ya kuwashinda Feisal Salum na Salum Abouhakari,’Sure Boy’ ,mchezaji bora baada ya kuwashinda Henock Inonga wa Simba nan a Fiston Mayele wa Yanga.
Ile tuzo yake ya tatu ni kuwa kwenye kikosi bora cha msimu hivyo tupo naye leo kwenye mwendo wa data namna hii:-
Dakika zake
Ameyeyusha jumla ya dk 2,074
Mechi
Ni mechi 23 za ligi amecheza
Kadi za njano
Ameonyeshwa kadi tatu za njano kwenye mechi za ligi
Timu ambazo zilisababisha akaonyeshwa kadi za njano ni KMC,Namungo na Biashara United.