WAKIWA kwenye maandalizi ya msimu wa 2022/23 washindi namba mbili kwenye Ligi Kuu Bara,Simba wameweka wazi kuwa wanatarajiwa kucheza mechi tatu za kirafiki.
Kwenye msimamo Simba ilimaliza ikiwa nafasi ya pili na pointi 61 baada ya kucheza mechi 30 za ligi.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa wanaendelea na maandalizi kwa ajili ya msimu mpya.
“Tunaendelea vizuri na maandalizi kwa ajili ya msimu mpya na kikubwa ni kuweza kuona kwamba tunapata kile ambacho tunastahili kwa msimu ujao.
“Kwa namna ambavyo tupo kwa sasa tuna mpango wa kucheza mechi tatu za kirafiki ikiwa makubaliano yatafikia kwa timu ambazo tunazungumza nazo.
“Ni Ismailia na timu ya Taifa ya Misri chini ya miaka 20 tunaweza kucheza nayo na katika mchezo wa tatu tutaiweka wazi timu ambayo tutacheza nayo mazungumzo yakikamilika,” amesema.
Miongoni mwa wachezaji waliopo kambini ni pamoja na Habib Kyombo,Meddie Kagere,Chris Mugalu,Pape Sakho