RASMI kiungo Augustine Okrah raia wa Ghana ametambulishwa ndani ya kikosi cha Simba.
Kiungo huyo alikuwa kwenye kikosi cha Bechem United ya Ghana na alifunga mabao 14 msimu wa 2021/22.
Nyota huyo ana uwezo wa kucheza katika nafasi ya winga kwa umakini mkubwa na kutimiza majukumu yake.
Ikumbukwe kwamba anakuwa ni mchezaji wa tatu wa kigeni kutambulishwa baada ya Moses Phiri na Victor Ackpan.
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano,Simba Ahmed Ally amesema kuwa mchezaji huyo ni mchezaji mwenye mafanikio na anakuja kufanya kazi.
“Tunaleta wachezaji wakubwa na wenye hadhi hivyo malengo ni kuona kwamba wanafanya vizuri kwenye mechi za kitaifa na kimataifa,” amesema.