Home Sports RAIS NI INJINIA NA MAKAMU NI ARAFAT

RAIS NI INJINIA NA MAKAMU NI ARAFAT

INJINIA Hersi Said kwa sasa ni rais wa kwanza ndani ya Klabu ya Yanga baada ya historia mpya kuandikwa.

Wanakuwa ni vingozi wa kwanza ndani ya Yanga aada ya kuingia kwenye mfumo wa mabadiliko na kuongozwa na rais ambapo zamani kiongozi mkubwa alikuwa ni Mwenyekiti.

Pia Mwenyekiti wa mwisho ndani ya Yanga yenye maskani yake Jangwani ni Mshindo Msolla ambaye ameweka wazi kuwa anajivunia kuwa sehemu ya mabadiliko.

Kwa upande wa rasi wajumbe waliweza kumpitisha Injinia Hersi bila kupigwa kwa kura za ndio huku mchuano ukiwa umebaki kwa makamu wake.

Makamu walikuwa wawili ambao wanagombea Arafat Haji na Suma Mwaitenda.

Baada ya kura kupigwa ni Arafat aliweza kupata ushindi kwa kuwa alikusanya kura 545 na Suma Mwaitenda kura 234 hivyo ni Arafat na Injinia watakuwa ni viogozi kwa miaka minne ijayo.

Previous articleKUPITIA KASINO YA MTANDAONI YA MERIDIANBET, SLOTI YA STICKY 777 INAWEZA KUKUPA FAIDA KUBWA!
Next articleMBWANA MAKATA APUNGUZIWA ADHABU YA KIFUNGO