Home Sports BREAKING:NYOTA WA KIMATAIFA ATAMBULISHWA YANGA

BREAKING:NYOTA WA KIMATAIFA ATAMBULISHWA YANGA

NYOTA wa kimataifa kutoka Burundi Gael Bigirimana ametambulishwa leo ndani ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Ni kiungo mshambuliaji Bigirimana ambaye yupo kwenye ardhi ya Tanzania kwa ajili ya kuwa na Wananchi ambao wameamua jambo lao.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Yanga imeeleza kuwa nyota huyu ni zawadi kutoka kwa rais wa kwanza wa Yanga ambaye ni Injinia Hersi Said.

Injinia amepitishwa kwa kura za ndio na wajumbe wote baada ya kukosa mshindani kwenye uchaguzi ambao umefanyika leo Julai 9,2022.

Previous articleVIDEO:ANGALIA MAZOEZI YA MSHAMBULIAJI MPYA WA SIMBA
Next articleKUPITIA KASINO YA MTANDAONI YA MERIDIANBET, SLOTI YA STICKY 777 INAWEZA KUKUPA FAIDA KUBWA!