Home Sports BEKI WA SIMBA INONGA AWEKA REKODI YAKE

BEKI WA SIMBA INONGA AWEKA REKODI YAKE

BEKI wa Simba,Henock Inonga ndani ya msimu wa 2021/22 ameweka rekodi yake ya kuwa mchezaji pekee aliyeonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa wale waliopenya kwenye orodha hiyo wakiwa wapo watatu.

Kesho kwenye ukumbi wa Rotana Hotel tuzo za Bodi ya Ligi zinatarajiwa kutolewa ambapo moja ya tuzo ambayo inatazamwa kwa ukaribu ni hii iliyokuwa mikononi mwa John Bocco wa Simba msimu wa 2020/21.

Inonga amecheza mechi 20 kafunga mabao matatu na ana kadi moja nyekundu ya moja kwa moja ambayo alionyeshwa kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Coastal Union uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Nyota mwingine ni Fiston Mayele wa Yanga ambaye ni mshambuliaji akiwa ametupia mabao 16 na pasi tano za mabao huku akiwa amecheza mechi zote 30 bila kuambulia kadi nyekundu wala njano.

Katumia dk 2,373 akiwa amehusika kwenye mabao 21 kati ya mabao 49 yalifungwa na timu hiyo.

Watatu ni Yannick Bangala kiungo huyu amecheza mechi 23 kayeyusha dakika 2,074 ana pasi moja ya bao na ameonyeshwa kadi za njano 3 kwenye ligi katika mechi tofauti.

Previous articleVIDEO:CEO YANGA AFUNGUKIA KUHUSU USAJILI,ATAJA WALIOLETA MATAJI
Next articleVIDEO:HAJI MANARA ASIMULIA ALICHOONGEA NA RAIS WA TFF