NYOTA watatu wanawania tuzo ya kiungo bora kwa msimu wa 2021/22 ambazo zinatarajiwa kufanyika Julai 7,2022 baada ya ligi kukamilika.
Mabingwa wameshajulikana ambao ni Yanga waliotwaa ubingwa baada ya kufikisha pointi 74 walipocheza mechi 30.
Viungo wote watatu kwa mujibu wa orodha iliyotolewa na Bodi ya Ligi Tanzania ni mali ya Yanga ambapo ni Feisal Salum,Salim Aboubhakar na Yannick Bangala.
Feisal msimu huu amecheza mechi 26 na kuyeyusha dk 2,071 akitupia mabao 6 na pasi 4 za mabao.
Bangala yeye amecheza mechi 23 ametumia dk 2,074.
Sure Boy akiwa ndani ya kikosi cha Yanga amecheza mechi 14 za ligi na ametoa pasi moja ya bao akiwa ametumia dk 1,033.