KIUNGO mshambuliaji wa Coastal Union, Abdul Suleiman, ‘Sopu’ ameweka wazi kwama walikuwa wanatambua umuhimu wa mchezo wa fainali dhidi ya Yanga jamo lililowafanya wacheze kwa kujituma huku akibainisha kwamba kilichowafanya washindwe kufanya vizuri ni mwendo wa majibizano hasa kila wanapofunga na wapinzani wao walikuwa wanafunga Julai 2,2022.
Nyota huyo alifunga hat trick kwenye mchezo huo na kuwa mchezaji bora na pia ni mfungaji bora katika Kombe la Shirikisho kwa kuwa amefunga jumla ya mabao 9