ANAANDIKA Haji Manara, Ofisa Habari wa Yanga:”Wapo walioidhihaki, na kuna wengine walinikejeli binafsi, wakasema sina jipya,nazikumbuka sana zile kashfa katika kituo kimoja cha Redio kuhusu kauli mbiu hii,walitumia wiki nzima kuiponda na kunishanbulia huku wakisema nawajaza Wananchi.
“Kuna nyakati hadi wenzangu klabuni wakanishauri tubadili,nikawaambia hii Slogan imenijia kwa kuwa tunahitaji kurudisha makombe yetu,tuendelee nayo hii hii hadi mwisho wa msimu, hii inatukumbusha wote nn tunataka msimu huu, wakanielewa.
RETURN OF THE CHAMPIONS, imelipa,tumebeba kila kitu walichokuwa nacho, tumerudisha makombe na heshima ya Club kwa kishindo kikuu.
“Asanteni Viongozi wote,Wadhamini wetu GSM, Wanachama na Mashabiki wote,bravo,(hongera) Wachezaji na enchi la ufundi.
“Haikuwa nyepesi ila imewezekana na sasa tunaangalia msimu ujao,tunamaliza uchaguzi wiki ijayo kisha tunakwenda pre season camp nje, tukirudi tunakuja na moto mkubwa, Insha’Allah tutatimiza malengo yetu tena na tena.
Nb: Tunaiomba Serikali wakati huu wa Pre season kuwe na mashindano haya
SENSA CUP NA ROYAL TOUR CUP.
Wengine ndio kazi zetu mjini, NA ASIKIMBIE MTU,
Byuti Byuti