KIUNGO MNIGERIA ASAINI AZAM FC

AZAM FC leo Julai Mosi wameufungua mwezi kwa kumtamulisha nyota mpya kwa ajili ya kuwa ndani ya kikosi hicho kwa msimu wa 2022/23.

Ni kiungo mkabaji kutoka Nigeria, Isah Ndala ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili.

Ndala alikuwa akichezea Plateau ya Nigeria, amesaini mkataba mbele ya mmiliki wa timu, Yusuf Bakhresa na Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin.

Kiungo huyo, mwenye umbo kubwa, sifa ya ukabaji na kupiga pasi, ni kwa ajili ya kuimarisha eneo la kiungo ndani ya Azam FC , ambapo Septemba mwaka huu atakuwa anatimiza umri wa miaka 20.

Aidha mbali na kucheza Plateau, Ndalla amepita pia katika timu ya Sevan ya Armenia na Nasarawa United ya Nigeria.

Huo unakuwa ni usajili wa tatu kuelekea msimu ujao, baada ya jana kuwatangaza nyota wawili kutoka Ivory Coast, Kipre Junior na Tape Edinho