Home Sports KIKOSI CHA SIMBA NDANI YA ARDHI YA DAR

KIKOSI CHA SIMBA NDANI YA ARDHI YA DAR

KIKOSI cha Simba leo kimewasili salama Dar kikitokea Songea ambapo kilikuwa na mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya Kwanza.

Sima chini ya Kocha Msaidizi Selaman Matola ilitoshana nguvu bila kufungana na Mbeya Kwanza katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Majimaji,Songea.

Matola amesema kuwa kukamilika kwa msimu huu wa 2021/22 ni mwanzo wa kujipanga kwa ajili ya msimu mpya wa 2022/23.

“Tumekamilisha mzunguko wa 2021/22 na sasa tunakwenda kufanya maandalizi kwa ajili ya msimu ujao na kwa wale ambao wamekuwa nasi ni jambo la kuwashukuru.

“Kila mmoja ameona namna ushindani ambavyo umekuwa mgumu na tuna amini kwamba kila mtu ameshuhudia hivyo tunawashukuru mashabiki kwa sapoti ambayo wamekuwa wakitupa,”amesema.

Ni pointi 61 ambazo Simba imekusanya baada ya kucheza mechi 30 kwa msimu wa 2021/22.

Previous articleKIUNGO ANDAMBWILE ASAJILIWA SINGIDA BIG STARS
Next articleKIUNGO MNIGERIA ASAINI AZAM FC