KIUNGO Novatus Dismas ambaye ni winga wa timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars ameweza kupata dili la kujiunga na Klabu ya Zulte Waregen.
Kiungo huyo aliwahi kucheza ndani ya kikosi cha Azam FC na alicheza pia katika Klabu ya Biashara United ambayo imeshuka daraja msimu wa 2021/22 baada ya kupoteza kwa kufungwa mabao 4-1 mbele ya Azam FC.
Timu hiyo ya Zulte Waregen ni ya Ubelgiji inashiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji.
Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) limemtumia salamu za pongezi kiungo huyo kwa hatua ambayo ameifikia huku yeye mwenyewe akiweka wazi Novatus akiweka wazi kwamba ni furaha kwake na hatua moja muhimu.