Home Sports BIASHARA UNITED WANAHITAJI MAOMBI

BIASHARA UNITED WANAHITAJI MAOMBI

UONGOZI wa Biashara United umewaomba mashabiki waweze kuiombea timu hiyo ili iweze kupata ushindi kwenye mchezo dhidi ya Azam FC ili iweze kufufua matumaini ya kubaki ndani ya ligi.

 Ofisa Habari wa Biashara United,Salma Thabit amesema kuwa nafasi ambayo wapo ni mbaya na wanahitaji ushindi mbele ya Azam FC leo.

Mchezo wa leo ni wa kufunga pazia kwa msimu wa 2021/22 na utakuwa ni wa mzunguko wa pili.

Kwenye msimamo Biashara United ipo nafasi ya 15 na pointi zake ni 28 ikipoteza mchezo wa leo itajihakikishia nafasi ya kushiriki Championship na ikishinda itakuwa na nafasi ya kucheza mchezo wa mtoano kutegemeana na matokeo ya mechi zitakavyokuwa.

Ni matokeo ya Ruvu Shooting v Prisons pamoja na mchezo wa Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar haya yatatoa picha ya nafasi ya Biashara United ya Mara.

“Tunaomba mashabiki waweze kutombea tuweze kushinda mchezo wetu kwa kuwa ni muhimu kupata matokeo na tunambua kwamba utakuwa mchezo mgumu.

“Abdulmajid Mangalo atakosekana kwenye mchezo dhidi ya Azam FC kwa kuwa alipata maumivu kwenye mchezo wetu uliopita dhidi ya KMC.

“Ni mchezo mgumu ambao utatoa nafasi ya kuweza kubaki kwenye ligi na tunajua kwamba hakuna wepesi katika mchezo huo ila tunaamini kwamba lolote linaweza kutokea,” alisema Salma

Previous articleMRITHI MIKOBA YA JOHN BOCCO KUJULIKANA
Next articleVIDEO:YANGA WAIPIGA DOGO KIMTINDO SIMBA