UWANJA WA SOKOINE:PRISONS 0-0 SIMBA

AKIWA ni miongoni mwa mastaa waliopo kwenye kikosi cha kwanza Kibu Dennis ameshuhudia ubao ukisoma Tanzania Prisons 0-0 Simba.

Ni kwenye mchezo wa ligi ambao kwa sasa ni mapumziko Uwanja wa Sokoine,Mbeya.

Kwa upande wa Prisons wamekuwa imara kwenye kuzuia mashambulizi ya Simba ambayo yanatengenezwa na kiungo huyo huku kazi ya Peter Banda ikiwa kwenye kujenga vibanda mbele ya Prisons nayo imekutana na ugumu kutoka kwa beki chipukizi Dotto Shaban.

Huu ni mchezo wa mzunguko wa pili na wa kuhitimisha mzunguko huu kwa msimu wa 2021/22 katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Simba 1-0 Tanzania Prisons.