Home Sports HII HAPA RATIBA YA LEO LIGI KUU BARA

HII HAPA RATIBA YA LEO LIGI KUU BARA

BAADA ya mabingwa Yanga kukabidhiwa ubingwa wao wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2021/22 mbele ya Mbeya City kwenye sare ya kufungana bao 1-1, Uwanja wa Sokoine bado ligi inaendelea.

Leo Juni 26, mechi mbili za mzunguko wa 29 zitachezwa ambapo kila timu inapambana kusaka pointi tatu muhimu.

Namungo FC itakuwa ugenini Uwanja wa Manungu ikimenyana na Mtibwa Sugar

Simba itakaribishwa na Tanzania Prisons, Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Mtibwa Sugar leo watakosa huduma ya kiungo Said Ndemla ambaye alionyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo dhidi ya Simba kwa kumchezea faulo Sadio Kanoute.

Previous articleYANGA Wafunga BARABARA, MSAFARA Wao HAUJAWAHI KUTOKEA, ANAIMBWA GSM tu HUKO, AZIZ KI Atajwa!
Next articleSIMBA YA SELEMAN MATOLA INAOGOPESHA