CEDRICK Kaze Kocha Msaidizi wa Yanga amesema kuwa hakuna mwalimu ambaye hatapenda kuwa na mchezaji kama Aziz KI kwa kuwa ni miongoni wa wachezaji wazuri.
Nyota huyo anatajwa kuibukia ndani ya kikosi cha Yanga akitokea Klabu ya ASEC Mimosas ambapo alikuwa anatajwa pia kwenye rada za Simba.
Kaze amesema kuwa suala la usajili lipo mikononi mwa viongozi ambao wanajua kipi kinatakiwa nao wanafanya yale ambayo yanahitajika.
“Nina amini kwamba uongozi wa Yanga unajua mahitaji yaliyopo na wanafanya usajili mzuri kwa ajili ya wakati ujao kitaifa na kimataifa.
“Mchezaji Aziz KI nina amini kwamba hakuna mwalimu ambaye hatapenda kuwa naye kwani ni mzuri hivyo ikiwa mambo yatakamilika basi tutajua,”.