MASTAA HAWA WAWILI YANGA KUIKOSA POLISI TANZANIA

 KUELEKEA mchezo wa kesho wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga dhidi ya Polisi Tanzania kuna nyota wawili wa Yanga ambao wanaweza kuukosa mchezo huo.

Yanga ni mabingwa wa ligi msimu wa 2021/22 wakiwavua taji hilo watani zao wa jadi Simba.

Kwa mujibu wa Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedrick kaze amesema kuwa wanatambua mchezo huo ni mgumu lakini watapambana kupata matokeo.

“Kwenye mchezo wetu tunaweza kuwakosa wachezaji wawili ambao ni Bakari Mwamnyeto yeye hajafanya mazoezi kwa muda mrefu baada ya kuumia lakini yupo vizuri.

“Djuma Shaban aliumia kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Coastal Union lakini naye amepata unafuu ameanza mazoezi hivyo ripoti ya daktari itaamua.

“Mchezo wetu utakuwa mgumu na ambacho tunakifanya ni kuona kwamba tunaweza kupata pointi tatu hasa ukizingatia kwamba hakuna ile presha ya ubingwa na sherehe zimeisha tunarudi kazini,” amesema.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza Polisi Tanzania ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na kuyeyusha pointi tatu mazima.