DICKSON Job beki wa Yanga ni mtu wa kazi ambapo kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Coastal Union wakati Yanga wakitangazwa kuwa mabingwa aliweza kuwa kwenye ubora.
Jumla alipiga pasi 80 na katika pasi hizo alizotoa ni moja pekee iliweza kupotea kwa kutofika mahali ambapo alikuwa anahitaji ifike.
Katika pasi hizo mguu ambao anapenda kuutumia ni ule wa kulia leo tupo naye hapa kwenye mwendo wa data namna hii ilikuwa Juni 15,2022:-
Pasi zake
Alitumia kichwa kupiga pasi 4
Mguu wa kulia alipiga pasi 72
Alipoteza pasi 1
Alitumia mguu wa kushoto kupiga pasi 4
Aliweza kukokota mpira mara 25
Alipewa jukumu la kupiga faulo mara 1
Kadi ya njano 0
Kadi nyekundu 0
Imeandikwa na Dizo Click