HAJI Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa kwa sasa licha ya kwamba bado hawajashinda ila ni suala la muda tu.
Leo Yanga ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Coastal Union ikiwa watashinda mchezo wa leo basi watakuwa ni mabingwa kwa kuwa pointi 67 ambazo watazipata hazitafikiwa na timu nyingine.
Manara amesema:”Nafasi yetu ya kushinda ubingwa ni kubwa sana kama 99%, bado hatujashinda ubingwa lakini nafasi ya sisi kuwa mabingwa ni kubwa sana, kwa mujibu ya msimamo wa ligi tunahitaji alama 3 ili tutawazwe kuwa mabingwa wa msimu huu.
“Mchezo wetu dhidi ya Coastal Union ni muhimu kwetu na tunajua kwamba ni timu imara lakini maandalizi ambayo yamefanyika ni makubwa tutapambana kupata pointi tatu muhimu,”.
Kwenye msimamo Yanga ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 64 huku Coastal Union ikiwa nafasi ya 6 na pointi 34.