NAHODHA wa timu ya Taifa ya England,Harry Kane amesema timu hiyo ina nafasi ya kushinda Kombe la Dunia 2022 litakalochezwa Novemba mwaka huu Qatar.
England imetwaa Kombe la Dunia mara moja tu ilikuwa ni mwaka 1966 na baada ya hapo imefanikiwa kuishia hatua ya nusu fainali mara mbili ilikuwa 1990 na 2018.
Kane amesema kuwa safari hii nchini Qatar wamepanga kufanya kweli.
“Hatujafanya vizuri katika michuano hii kwa muda mrefu lakini nadhani kwamba ni sahihi kuwa na mawazo kwamba tunaweza kwenda kwenda na kujaribu kushinda kombe hilo,” amesema.
Jana England ilipoteza kwa kufungwa mabao 4-0 dhidi ya Hungary Nations League.