MASTAA HAWA WAMEANZA KUONYESHA MAKEKE JIONI

    MUDA wa mahesabu wapo ambao huwa hawajali itakuaje zaidi ya kuendelea kupambana mpaka wanafikia lengo lao wakiamini kwamba anayecheka mwisho huwa na furaha zaidi.

    Kuna mastaa msimu wa 2021/22 kwao walianza kwa kusausa na sasa ligi ikiwa inakaribia kumeguka kwa shimo limeanza kutema jioni kabisa namna hii:-

    Jeremia Juma

    Staa wa kwanza kufunga hat trick ndani ya ligi msimu huu wa 2021/22 ilikuwa mbele ya Namungo FC, baada ya kufunga na kufikisha mabao 5, miguu ilipata kigugumizi kufunga kwenye mechi alizocheza.

    Ilikuwa Novemba 27,2021 alipoweza kufunga na kaibuka kwa kuwatungua Geita Gold, Mei 25 Uwanja wa Sokoine na kufikisha mabao 6.

    John Bocco

    Ana kazi ya kutetea kiatu cha ufungaji bora ambapo msimu uliopita alifunga mabao 16, mwanzo wa msimu hakuwa kwenye ubora wake na mchezo wa kwanza kwa Simba alikosa penalti mbele ya Biashara United.

    Ngoma sasa imepamba moto aliuwasha kwa mara ya kwanza Mei 8,2022 mbele ya Ruvu Shooting kisha akafunga mbele ya Kagera Sugar na Azam FC na kufikisha mabao 3.

    Yusuph Mhilu

    Kijana yupo zake ndani ya Simba akiwa ni mshambuliaji ambaye hajafunga lakini ni pasi moja ya bao katoa kwenye ligi kwa mara ya kwanza ilikuwa mbele ya Ruvu Shooting, Mei 8,2022 alimpa nahodha wake John Bocco.

    Matheo Anthony

    Mshamuliaji huyu wa KMC aliweza kutupia mabao manne mwanzoni mwa msimu na mchezo wake wa mwisho kufunga ilikuwa ni mbele ya Mbeya Kwanza, Uwanja wa Sokoine kisha ukame wa mabao ukawa unaishi kakwe.

    Aliibuka Mei 12 alipofunga mabao 2 mbele ya Mtibwa Sugar na akafunga bao lake la 7 mbele ya Mbeya City ikiwa ni muda wa kufunga hesabu za msimu.

    Kichuya

    Shiza Kichuya alianza msimu kwa kasi ambapo mchezo wa kwanza mbele ya Geita Gold,Septemba 27,2021 aliweza kupachika bao la kwanza kwenye ligi isha mambo yakawa yanasuasua.

    Mzunguko wa pili kaja kivingine ambapo aliweza kuwatungua Yanga bao moja na walipocheza na Simba, Uwanja wa Ilulu alitoa pasi kwa pigo la kona lilifungwa na Jacob Masawe mbele ya Biashara United Mei 17 alitupia kambani mbili mwamba huyu.

    Heritier Makambo

    Mei 20,2022 alifunga bao lake la kwanza ndani ya ligi kwa msimu wa 2021/22 akiwa na Yanga kwenye ligi baada ya kurejea kwa mara nyingine Bongo.

    Prince Dube

    Aliwaka msimu wa 2020/21 kwa kutupia mabao 14 ndani ya ligi akiwa na Azam FC, kutokana na uwa nje akitibu majeraha ilikuwa ngumu kwake kuwaka msimu huu wa 2021/22.

    Ni bao moja analo kibindoni alifunga mbele ya Namungo ilikuwa Machi 16,2022 Uwanja wa Ilulu wakati ligi inakaribia kufika ukingoni aliweza kutoa pasi ya bao ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya KMC ilikuwa Mei 7,2022 alimpa Ayoub Lyanga aliyepachika bao dk ya 1.

    Emannuel Martin

    Yupo zake ndani ya Dodoma Jiji, Machi 13,2022 aliweza kufunga bao mbele ya Mbeya Kwanza, Uwanja wa Jamhuri Aprili kwake ilikuwa nzito kwa kuwa hakufunga.

    Ilibidi asubiri mpaka Mei 20 alipoweza kutoa pasi ya bao kwa Anuary Jabir ambaye alifunga bao dk ya 23 mbele ya Coastal Union.

    Ambundo

    Winga huyu aliweza kutupia bao lake la kwanza mbele ya Polisi Tanzania ilikuwa Januari 23,2022  ilibidi asubiri mpaka Mei 15 alipofunga mbele ya Dodoma Jiji kisha akafunga bao lake la tatu mbele ya Mbeya Kwanza ilikuwa ni Mei 20.

    Kaanza kuingia chimbo na kutoa madini kwenye miguu yake ikiwa ni jioni kabisa wakati ligi inakariia kumeguka kwa msimu wa 2021/22

    Sure Boy

    Salum Aboubhakari, Mei 20,2022 Uwanja wa Mkapa aliweza kutoa pasi yake ya kwanza akiwa na kikosi cha Yanga kwenye ligi alimpa mshikaji wake Fiston Mayele.

    Ilikuwa kwenye ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Mbeya Kwanza,kaanza kufanya yake ikiwa ni jioni kabisa.

    Previous articleUEFA NATIONS LEAGUE KUFIKIA TAMATI WIKIENDI HII, UNAMALIZAJE?
    Next articleMJUE STAA YANGA AMBAYE AMELETWA NA AUCHO,CHAMPIONI JUMAMOSI