MANCHESTER CITY WAMTAKA SAKA

IMEELEZWA kuwa mabingwa wa Ligi Kuu England, Manchester City wanahitaji saini ya staa wa Arsenal, Bukayo Saka katka kipindi cha miaka miwili ya mwisho ya mkataba wake.

City wanahitaji kumpata nyota huyo ili aweze kuondoka ndani ya kikosi cha Arsenal kinachonolewa na Kocha Mkuu, Mikel Arteta.

Inaelezwa kuwa City pamoja na wapinzani wao wakubwa Liverpool wote wanamtazama staa huyo wa Arsenal ili awe hazina kubwa hapo baadaye kutokana na kipaji chake.

Hata hivyo kushindwa kufuzu mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kumeongeza nguvu ya nyota huyo kuweza kusepa hapo Arsenal.