Home Sports TAIFA STARS KUVAA NIGER LEO

TAIFA STARS KUVAA NIGER LEO

KIM Poulsen, Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo wa kuwania kufuzu AFCON 2023.

Jana Mei 3,2022 wachezaji wa Timu ya Taifa,Taifa Stars, walifanya mazoezi ya mwisho Stadium L’amitié General Matthieu KEREKOU, Cotonou, Benin kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Kundi F kufuzu AFCON dhidi ya Niger utakaochezwa leo Juni 4, 2022.

Kim amesema kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu lakini wapo tayari hasa kutokana na maandalizi ambayo wameyafanya.

“Ni mchezo wenye ushindani na kila timu inahitaji ushindi hivyo ambacho tutakifanya ni kutafuta ushindi tupo tayari kwa ajili ya hilo,”.

Miongoni mwa mastaa ambao wapo kwenye kikosi cha Stars ni pamoja na Mbwana Samatta, Mzamiru Yassin,Simon Msuva.

Previous articleKUNA WINGA YANGA ALITISHIWA KUROGWA
Next articleMWENDO WA BIASHARA UNITED NA MBEYA KWANZA UNA JAMBO LAO